Orodha ya majina ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na shule za kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2026 ni suala linalosubiriwa kwa umuhimu mkubwa na wahitimu wa elimu ya sekondari nchini Tanzania.
Kufuatia kukamilika kwa mtihani wa kidato cha nne, wanafunzi, wazazi, na walezi hufuatilia kwa karibu taarifa rasmi kuhusu upangaji wa wanafunzi katika ngazi hii ya elimu ya juu ya sekondari. Hatua hii ni muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi, ikitoa fursa ya kupata elimu katika mazingira yanayowaandaa kwa masomo ya elimu ya juu na hatimaye, ulimwengu wa kazi.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hufanya mchakato wa upangaji wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano.
Upangaji huu huzingatia matokeo ya kitaaluma ya wanafunzi, machaguo yao ya masomo, na upatikanaji wa nafasi katika shule husika. Ni muhimu kwa wadau wote wanaohusika kufahamu taratibu za kupata taarifa hizi muhimu.
Makala haya yanatoa mwongozo rasmi kuhusu namna ya kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2026. Mchakato huu unaendeshwa kwa uwazi, na taarifa zote muhimu hutolewa kupitia chaneli rasmi za serikali. Kupitia makala hii, wasomaji watapata maelezo ya kina kuhusu vigezo vya upangaji, hatua za kuangalia matokeo, na taratibu zinazofuata baada ya mwanafunzi kupangiwa shule, kwa lengo la kuhakikisha maandalizi bora ya safari ya elimu ya sekondari ya juu.
Mchakato wa Kuchaguliwa Kidato cha Tano 2026
Mchakato wa kuchagua wanafunzi wataojiunga na shule za serikali za kidato cha tano unaendeshwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambayo hutangaza majina ya wanafunzi na shule walizopangiwa kidato cha tano 2026.
Wanafunzi hupangiwa shule kulingana na vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na alama walizopata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne, chaguo la tahasusi alilochagua, na nafasi zilizopo katika shule hizo.
Kwa mwaka 2026, wanafunzi wanaotaka kuona majina yao wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI na kufuata hatua rahisi za kutafuta matokeo yao. Hapa tunatoa mwongozo wa hatua kwa hatua ili uweze kujua kama umechaguliwa.
Jinsi ya Kuangalia Majina na Shule Zilizopangiwa
- Tembelea tovuti rasmi: https://selform.tamisemi.go.tz/ au moja kwa moja https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation.

- Chagua chaguo la First Selection (au version inayofaa, kama Second Selection ikiwa imetolewa).
- Tafuta kwa kutumia:
- Jina la mwanafunzi (Candidate Name).
- Shule ya awali (Examination Center).
- Au chagua mkoa/shule moja kwa moja ili kuona orodha kamili.
- Orodha ina majina ya wanafunzi, shule walizopangiwa, na mara nyingi combination au maelezo mengine.


Ikiwa unatafuta orodha kamili (PDF au full list kwa mikoa yote), nenda moja kwa moja kwenye Selform na uchague chaguo la kutazama shule zote. Baadhi ya majina huwa yanapatikana katika PDF kwenye tovuti ya TAMISEMI au kurasa zinazohusiana.
Vigezo Vinavyotumiwa na TAMISEMI Kufanya Uchaguzi
Serikali hutumia vigezo madhubuti katika kuchagua wanafunzi watakaopata nafasi za kujiunga na kidato cha tano. Baadhi ya vigezo muhimu ni pamoja na:
- Ufaulu wa Masomo Yasiyopungua Matatu: Mwanafunzi anapaswa kuwa na alama za A, B au C katika masomo yasiyo ya dini.
- Alama ya Ufaulu Katika Masomo ya Tahasusi: Mwanafunzi anapaswa kuwa na alama za angalau A, B au C katika masomo yake ya tahasusi.
- Ushindani wa Nafasi: Uchaguzi unafanyika kulingana na upatikanaji wa nafasi katika shule husika.
- Umri wa Mwanafunzi: Mwanafunzi anapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 25 ili kujiunga na kidato cha tano.
Uchaguzi wa Kwanza na Uchaguzi wa Pili
Baada ya majina kutangazwa, wanafunzi waliochaguliwa huorodheshwa kwenye awamu mbili za uchaguzi: First Selection (Uchaguzi wa Kwanza) na Second Selection (Uchaguzi wa Pili).
Uchaguzi wa Kwanza
Hii ni orodha ya kwanza ya wanafunzi waliofanikiwa kupata nafasi katika shule za kidato cha tano. Wanafunzi hawa huchaguliwa kwa kuzingatia ufaulu wao wa juu kitaaluma, machaguo yao ya masomo, na upatikanaji wa nafasi katika shule walizoomba.
Wanafunzi ambao majina yao yanaonekana kwenye orodha hii wanapaswa kuchukua hatua zifuatazo:
- Kupakua na kuchapisha barua ya kujiunga (Joining Instructions) kutoka kwenye tovuti ya shule waliyopangiwa au kupitia tovuti ya TAMISEMI (https://selform.tamisemi.go.tz).
- Kuandaa mahitaji yote muhimu yaliyoainishwa kwenye barua ya kujiunga, kama vile sare za shule, vifaa vya masomo, na ada (ikiwa inahitajika).
- Kuripoti kwenye shule waliyopangiwa ndani ya muda uliowekwa. Kukosa kuripoti kwa wakati kunaweza kusababisha kufutwa kwa nafasi hiyo.
Uchaguzi wa Pili: Ikiwa mwanafunzi hakupata nafasi katika awamu ya kwanza, anaweza kufuatilia uteuzi wa awamu ya pili. TAMISEMI hufanya uteuzi huu kwa wanafunzi ambao walikidhi vigezo lakini hawakupata nafasi awali kutokana na ushindani au nafasi ndogo.
Orodha ya uteuzi wa pili kwa kawaida hutolewa baada ya muda mfupi kufuatia orodha ya kwanza yenye majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano. Taarifa kuhusu uteuzi huu itapatikana kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI
Jinsi ya Kuangalia Updates za Second Selection
Angalia kurasa za elimu kama Mabumbe, Waza Elimu, au Facebook groups za Form Five Selection kwa updates za haraka (lakini thibitisha na chanzo rasmi).
Tembelea moja kwa moja: https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation
Chagua “Selection Version” na angalia kama chaguo jipya la Second Selection limeongezwa.
Tumia search kwa jina la mwanafunzi, shule ya mtihani (center), au tafuta orodha kwa mkoa.
Angalia tovuti kuu ya TAMISEMI: https://tamisemi.go.tz/
Nenda sehemu ya “Habari” au “Matangazo” kwa taarifa mpya. Wanapotoa Second Selection, huwa wanatangaza na kiambatisho (attachment) au link.
Ikiwa haijapatikana bado:
Subiri wiki chache – mara nyingi inategemea idadi ya nafasi zilizo wazi baada ya kujiunga kwa awamu ya kwanza.
Kwa maelezo zaidi au updates:
Ikiwa ni selection ya Zanzibar, angalia MOEZ (Ministry of Education Zanzibar), lakini kwa Tanzania Bara ni TAMISEMI.
Tovuti kuu ya TAMISEMI: https://tamisemi.go.tz/ (angalia taarifa za hivi karibuni kuhusu “Machaguo ya Kidato cha Tano”).
makala zaidi:






2 Comments