Home / UDAKU / “Michezo ya kuteleza kwenye theluji kwa mtindo huru katika Olimpiki za Majira ya Baridi 2026.”

“Michezo ya kuteleza kwenye theluji kwa mtindo huru katika Olimpiki za Majira ya Baridi 2026.”

Michezo ya kuteleza kwenye theluji kwa mtindo huru Olimpiki za Majira ya Baridi 2026 ni moja ya michezo maarufu katika Olimpiki za Majira ya Baridi 2026. Mchezo huu unahusisha wanariadha kufanya mbinu za kiufundi angani, kuruka, na kutua kwa ustadi mkubwa. Mashindano haya yanajumuisha aina kama moguls, aerials, ski cross, slopestyle, na halfpipe. Freestyle skiing huvutia mashabiki wengi kutokana na ubunifu, kasi, na hatari yake.

Michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi 2026, imefunguliwa rasmi Februari 6-22 katika miji miwili ya Italia ya Milan-Cortina. Programu ya michezo hiyo iliyopewa jina la Milan-Cortina tayari imeanza siku ya Jumatano.

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026

Picha hii ilipigwa Februari 6, 2026 inaonyesha pete tano za Olimpiki kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa San Siro, mjini Milan, Italia. (Xinhua/Chen Yichen)

Michuano ya Olimpikiya majira ya baridi 2026, imefunguliwa rasmi Februari 6-22 katika miji miwili ya Italia ya Milan-Cortina.

Hafla ya ufunguzi inafanyika Ijumaa na kujumuisha maonyesho kutoka maeneo yote ya mashindano, huku wanariadha 2,900 wakipita karibu na viwanja wanavyoshindania.

Sherehe hizo za ufunguzi zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio. Marekani inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michezo ijayo ya majira ya joto mwaka 2028 huko Los Angeles.

Programu ya michezo hiyo iliyopewa jina la Milan-Cortina tayari imeanza siku ya Jumatano huku Marekani ambayo ni bingwa mtetezi ikichukua uongozi tayari katika baadhi ya vipengele.

Moto wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026 umewashwa katika uwanja wa Angelo Dibona, Cortina, Italia, Februari 6, 2026. (Xinhua/Fei Maohua)

Rais wa Italia, Sergio Mattarella, anatangaza rasmi ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa San Siro, mjini Milan, Italia, Februari 6, 2026. (Xinhua/Li Ming)

Wasanii wakicheza kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa San Siro, mjini Milan, Italia, Februari 6, 2026. (Xinhua/Cheng Min)


Usalama waimarishwa 

Kuelekea michezo hiyo, mamlaka za Italia zimeimarisha ulinzi kuelekea ufunguzi wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Milan–Cortina, ikisambaza maelfu ya maafisa kuhakikisha usalama wa wanamichezo, watazamaji na viongozi wa dunia katika maeneo mbalimbali kuanzia Milan hadi milima ya Dolomites.

Siku moja kabla ya ufunguzi, Baraza la Waziri Mkuu Giorgia Meloni lilipitisha amri mpya ya usalama yenye masharti makali zaidi ili kukabiliana na maandamano yanayoweza kuzuka, hatua ambayo imekosolewa na baadhi ya wabunge wa upinzani wakidai inabana uhuru wa kujieleza.


3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *